Chibada kupandishwa timu ya wakubwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2020
Chibada kupandishwa timu ya wakubwa

Baada ya kuonyesha 'shoo ya kibabe' kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon, benchi la ufundi la klabu ya Yanga limeahidi kumtumia Omary Chibada katika mechi za ligi na mashindano mengine

Juzi ilikuwa mara yake ya kwanza Chibada kuitumikia timu ya wakubwa akipewa nafasi hiyo na kocha Cedric Kaze baada ya kumshuhudia kwenye mazoezi ya kikosi cha Yanga B

Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema, kiwango alichoonyesha Chibada juzi, kimewapa sababu ya kumtumia zaidi kwenye kikosi cha kwanza

Pamoja na kucheza kwa dakika chache, Chibada alionyesha uwezo mkubwa sana eneo la kiungo akipiga pasi makini

Hii ni nafasi kwake kumshawishi Kaze ili aweze kumpa nafasi zaidi uwe mwanzo mzuri wa safari yake ya mafanikio kwenye soka

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’