Nyota mpya wa Yanga Saido Ntibazonkiza amefichua kuwa klabu ya Simba ilijaribu kumshawishi aachane na Yanga aweze kujiunga nao
Ntibazokinza aliyefunga mabao manne katika mechi tatu zilizopita akiwa na timu ya Taifa ya Burundi, amefichua kuhusu kufuatwa na Mawakala wa Simba
"Nilifuatwa na watu wa Simba wakitaka nijiunge nao, nakuwa niwaeleze nalipwa kiasi gani, wao watanilipa vizuri zaidi"
"Sikuwa tayari kukubaliana nao kwa kuwa tayari nimeshasajiliwa na Yanga na hata kiasi cha malipo ninayolipwa na Yanga ni siri yangu na klabu. Nilitoa taarifa kwa uongozi juu ya watu hawa wanaonisumbua," alisema Ntibazonkiza
"Binafsi sitaki kuumiza mioyo ya mashabiki wa Yanga, wamenipokea vizuri na mimi niko tayari kuwatumikia"
Ntibazonkiza alisajiliwa na Yanga mwezi uliopita akiwa mchezaji huru akisaini mkataba baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya Burundi yeye akiwa mfungaji wa bao pekee la Burundi waliofanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Ni usajili uliopendekezwa na kocha Cedric Kaze, alipaswa kujiunga na Yanga mapema zaidi kabla ya kuanza msimu huu
Anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanza majukumu yake ndani ya kikosi cha Yanga
Ataanza rasmi kuitumikia Yanga Disemba 15 dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa