Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo amesema sababu iliyopelekea mchezo wa kesho wa marudiano wa kufuzu fainali ya Afrika dhidi ya Tunisia kuchezwa saa 4 usiku ni kutokana na utaratibu ulielekezwa na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).
Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa saa 10 jioni lakini CAF wametoa utaratibu kuwa unapaswa kuchezwa saa nne usiku.
Singo amesema CAF wametoa utaratibu kuwa mashabiki wanapaswa kuingia asilimia 50 ambapo watapaswa kuingia 30,000 kulikngana na ukubwa wa uwanja ingawa Serikali imesema watauza tiketi kwa mashabiki 20,000 pekee.
Mkurugenzi huyo ameweka wazi pia mashabiki watakaa kwa kupeana nafasi (Social Distance) na kufuata sheria zote za kujikinga na COVID 19/huku ulinzi ukiwa umeimarishwa ndani na nje ya uwanja.