Kesho Jumanne timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Tunisia katika mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya michuano ya Afcon 2021, kundi J
Stars na Tunisia zilichuana siku tatu zilizopita nchini Tunisia na wenyeji Tunisia kuondoka na ushindi wa bao 1-0

Waamuzi kutoka nchini Msumbiji wanatarajia kuchezesha mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa nne usiku
Mashabiki 30,000 wameruhusiwa kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo huo ambao viingilio vilivyopangwa VIP ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-

ADVERTISE HERE