Kuanzia msimu uliopita, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilibadili kalenda ya kufunguliwa dirisha dogo la usajili kutoka Novemba 15 na kuwa Disemba 15
Msimu uliopita dirisha lilifunguliwa Disemba 15 na hivyo hivyo, TFF imethibitisha kuwa msimu huu hakutakuwa na mabadiliko
Mpaka sasa Yanga tayari imeshasajili mchezaji mmoja Sadio Ntibazonkiza ambaye ataanza kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria pale dirisha la usajili litakapofunguliwa
Inaelezwa Yanga itaongeza nyota wengine wawili dirisha la usajili litakapofunguliwa
ADVERTISE HERE