Hongera watani zetu kwa hatua mliyofikia

Admin By Admin
β€’
4 Dec 2017
Hongera watani zetu kwa hatua mliyofikia
Yanga na Simba ni vilabu vikongwe zaidi nchini Tanzania. Kwa miaka mingi timu hizi zimekuwa zikimilikiwa na wanachama.

Aidha uendeshaji wake umekuwa wa kutegemea zaidi wafadhili na michango ya wanachama kwa kuwa zimekuwa hazijiendeshi kibiashara.

Lakini hatua iliyofikiwa na watani wetu Simba ya kubadili Katiba yao na kuifanya timu yao ijiendeshe kibiashara si ya kubezwa hata kidogo.

Naamini mwekezaji waliompata jana, Mohammedi Dewji ambaye anamiliki hisa kwa asilimia 50 kwa kushirikiana na wanahisa wengine wataweza kufanya mabadiliko ya kweli katika klabu hiyo.

Bila shaka wataanza kufanya mambo yao kwa weledi na huo huenda ukawa mwanzo wao wa mafanikio.

Wakati wenzetu wakipiga hatua hiyo nasi hatuna budi kujitafakari. Hakuna shaka kuwa Yanga nayo inahitaji mabadiliko katika uwendeshaji wake ili kuendelea kuwa mbabe wa soka la Tanzania.

Mabadiliko yataiondoa timu kutoka katika utegemezi wa watu na hivyo ndivyo uendeshaji wa soka la kisasa unataka.

Tukiendelea kuamini kwamba tutafanikiwa kwa mfumo huu huu tulioanao tutakuwa tunajidanganya.

Changamoto zinazoikumba klabu kwa sasa ndio iwe chachu ya kuyafuata mabadiliko.

Ni wakati muafaka kwa WanaYanga kushinikiza viongozi wao waende na wakati.

Natambua Yanga pengine ingekuwa ya kwanza kufanya mabadiliko lakini imekuwa ikikumbana na vikwazo kila inapoanza mchakato.

Jambo hilo linagharama yake. Lazima ifike muda wanachama wa Yanga wakabadili fikra zao, wakubaliane na uhalisia wa wakati.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
24m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
49m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’