Mukoko Tomombe : Tuzo zinamiminika kabatini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Nov 2020
Mukoko Tomombe : Tuzo zinamiminika kabatini

Kiungo Mukoko Tomombe ameendelea kujizolea tuzo nchini jana akitwaa tuzo wa mchezaji bora wa mwezi Oktoba Ligi kuu ya Vodacom

Mcongomani huyo amenza vyema katika kikosi cha Yanga, huu ni usajili uliolipa mapema sana

Ndani ya Yanga tayari amezoa tuzo nne. Mchezaji bora wa mechi mara mbili, mchezaji bora wa mwezi Septemba lakini pia katika mchezo dhidi ya Simba Mukoko aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo

Tuzo ya VPL inakuwa tuzo ya tano kuipata katika kipindi cha miezi mitatu tu aliyoitumikia Yanga mpaka sasa

Huu ni usajili ambao thamani yake yake imeonekana mapema sana

Awapo uwanjani, Mukoko ni mpambanaji, mhamasishaji, anakuwa mstari wa mbele kuhakikisha timu inafanikisha malengo ya kupata matokeo katika kila mchezo

Amefunga mabao matano, mawili kwenye ligi na matatu kwenye mechi za kirafiki

Haishangazi kuona kocha Cedric Kaze amemchagua kuwa moja ya manahodha katika kikosi chake akisaidiana na Lamine Moro ambaye ndiye nahodha namba moja na Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye ni nahodha wa pili

Mukoko amewahakikishia Wanayanga kuwa yeye ni Mwananchi na hao wanaozusha kumsajili watasubiri sana...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’