Tanzania imepoteza mchezo wa pili ugenini katika kampeni ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afcon 2021 wakifungwa bao 1-0 dhidi ya Tunisia
Bao pekee la Tunisia lilifungwa na Youssef Msakni kupitia mkwaju wa penati kwenye dakika ya 18
Tunisia ilikuwa bora kwa muda wote wa mchezo huku Stars wakilazimika kujilinda kwa muda mwingi, mlinda lango Aishi Manula akiokoa nafasi kadhaa za wazi
Kwa matokeo hayo, Stars italazimika kushinda mchezo wa pili dhidi ya Tunisia ambao utapigwa Novemba 17 uwanja wa Benjamin Mkapa
Matokeo tofauti na ushindi katika mchezo huo yanaweza kufifisha matumaini ya kucheza fainali za Afcon 2021
ADVERTISE HERE