Kaze, Mukoko washinda tuzo za VPL Oktoba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2020
Kaze, Mukoko washinda tuzo za VPL Oktoba

Kocha wa Young Africans SC ya Dar es Salaam, Cedric Kaze, amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Oktoba msimu wa 2020/21.

Kaze aliwashinda Aristica Cioaba wa Azam FC na Francis Baraza wa Biashara United ambapo Kaze aliiongoza Yanga katika michezo mitatu na kushinda yote.

Yanga chini ya Kaze ilizifunga Polisi Tanzania, KMC na Biashara United na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Cioaba aliiongoza Azam kushinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza moja, huku Baraza akiiongoza Biashara kushinda michezo mitatu na kupoteza miwili ikipanda kutoka nafasi ya saba hadi ya nne.

Wakati huohuo, Kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba msimu wa 2020/21.

Mwezi huo wa Oktoba, Yanga ilicheza michezo minne, ikiwa ndiyo timu iliyoshinda michezo yake yote na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom inayoshirikisha timu 18.

Yanga ilizifunga Coastal Union 3-0, Polisi Tanzania 1-0, KMC 1-2 na Biashara United, 0-1 ambapo Mukoko alitoa mchango mkubwa katika ushindi huo ikiwa ni pamoja na kufunga bao moja dhidi ya Polisi Tanzania.

Mukoko aliwashinda mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube na mshambuliaji wa Gwambina FC, Meshack Abraham aliongia nao fainali, ambapo Dube aliiongoza Azam kubaki kileleni baada ya kuvuna pointi 10 katika mwezi huo, ikishinda tatu, sare moja na kupoteza moja, huku mshambuliaji huyo akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za usaidizi wa mabao.

Kwa upande wa Meshack aliiongoza Gwambina kupata pointi nane ikishinda michezo miwili, sare miwili na kupoteza mmoja, ikipanda kutoka nafasi ya 17 hadi ya 14 akiifungia timu yake mabao manne.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
26m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’