Mashabiki, wapenzi na Wanachama wa Yanga keshokutwa Jumapili wana jambo lao pale uwanja wa Azam Complex Chamazi pale kikosi chao kitakaposhuka dimbani kupepetana na African Lyon ukiwa ni mchezo wa kirafiki
Ni kwa kiingilio cha 3,000 mzunguko na 5,000 VIP. Baada ya kukosekana uwanjani kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha, Carlinhos anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Cedric Kaze kitakachowapa burudani mashabiki wa Yanga
Mchezo huu ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Novemba 22
ADVERTISE HERE