Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema wachezaji Mukoko Tomombe na Tuisila Kisinda wana mikataba ya miaka miwili kila mmoja
Aidha Hersi amesema nyota hao wana furaha Yanga, hizo tetesi zinazoendeshwa kwenye mitandao ya kijamii ni porojo tu
Baada ya tetesi za Chama kuhusishwa na Yanga kushika kasi, Msemaji wa Simba Haji Manara ane akaibuka na tetesi zake akidai wamekusudia kuwan'goa Mukoko na Kisinda
"Niwahakikishie mashabiki wa Yanga na wapenzi wa mpira wa miguu nchini, Mukoko na Kisinda wote wana mikataba ya miaka miwili na Yanga"
"Kila kitu kipo sawa na wachezaji hawa. Mukoko ni nahodha wetu wa tatu na anafurahia maisha ndani ya klabu ya Yanga, " alisema Hersi
Mukoko na Kisila walitua Yanga mwezi August wakitokea klabu ya AS Vita. Injinia Hersi alikwenda DR Congo mwenyewe kukamilisha usajili wa wachezaji hawa akipata baraka zote kutoka kwa klabu ya AS Vita na Meneama ambayo ilikuwa inammiliki Kisinda