Ubingwa utaletwa na matokeo mazuri - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2020
Ubingwa utaletwa na matokeo mazuri - Kaze

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema kwa sasa mkakati wake ni kuhakikisha timu yake inafanya vizuri katika kila mchezo unaokuja mbele yao

Kaze amesema pamoja na mwendelezo mzuri wa timu yake katika ligi wakiwa hajawapoteza mchezo hata mmoja, bado anaona wana kazi ya kufanya kuweza kufikia malengo

"Ni kweli lengo letu ni kuona tunatwaa ubingwa msimu huu, lakini niseme ukweli ligi bado, ni mapema sana kwa sasa kuanza kujiweka kifua mbele tutatwaa ubingwa, sio kwa Yanga tu hata kwa timu nyingine, muda bado sana," alisema Kaze.

Kocha huyo alisema wataanza kuona uwelekeo wao wa kutwaa ubingwa kuanzia katika mzunguko wa pili wa ligi.

"Kama tutamaliza hivi mzunguko wa kwanza, na tukaanza mzunguko wa pili kama tulivyoanza mzunguko wa kwanza, baada ya michezo kadhaa tunaweza tukaongelea mwenendo wetu kuelekea kwenye ubingwa, kwa sasa nataka wachezaji wangu waweke umakini katika kila mchezo tunaocheza," aliongeza Kaze.

Yanga ilianza mazoezi jana ikiwa na kikosi cha wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za taifa. Nyota nane wa Yanga wameitwa timu za Taifa, saba Tanzania na mmoja Rwanda

Yanga imecheza michezo 10 na kushinda michezo saba, huku ikitoka sare mara tatu ukiwamo mchezo dhidi ya watani zao Simba, uliochezwa wiki iliyopita. Pia walilazimishwa sare mechi dhidi ya Tanzania Prisons na Gwambina Fc

Katika msimamo wa ligi, Yanga yenye pointi 24 iko kwenye nafasi ya pili nyuma ya vinara Azam FC wenye pointi 25 wakati mabingwa watetezi, Simba wako katika nafasi ya tatu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’