Baada ya tetesi za usajili wa mchezaji Clatous Chama 'kubamba' mitandao ya kijamii wiki hii, leo upande wa pili nao wamekuja na propaganda wakidai kutaka kumn'goa kiungo mkabaji Mukoko Tomombe na winga Tuisila Kisinda
Kumekuwa na upotoshaji mkubwa unaofanywa zikiibuliwa taarifa kuwa wachezaji hao wanaitumikia Yanga kwa mkopo
Kisinda na Mukoko walipotua nchini kuitumikia Yanga, wakala wao alitoa ufafanuzi na kuthibitisha kuwa wote walisaini mikataba ya miaka miwili miwili
Mukoko alikuwa mchezaji AS Vita, GSM walinunua mkataba wake wa mwaka mmoja na nusu uliokuwa umebaki
Kwa upande wa Kisinda, yeye alikuwa akiitumikia AS Vita kwa mkopo akitokea klabu ya Meneama United
Kabla ya kumpa mkataba wa miaka miwili, Yanga walimalizana na Meneama kisha wakamalizana na AS Vita ambao walikuwa wamempa mkataba wa mkopo wa miaka miwili
Ni kama propaganda hizi zimeibuliwa ili kuwapoza mashabiki wa Simba ambao bado hawana uhakika kama watamuona Chama katika timu yao msimu ujao