Tusiyumbishwe na habari za mitaani - Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Nov 2020
Tusiyumbishwe na habari za mitaani - Dk Msolla

Mwenyekiti wa klau ya Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka wapenzi na Wanachama wa klabu hiyo kuwa watulivu wakati Mshauri wa klabu Senzo Mazingisa akihojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuihujumu Simba

Akizungumza mbashara kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Yanga, Dk Msolla amesema uongozi wa Yanga unaamini Senzo hakufanya kosa lolote na watakuwa tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika na Jeshi la Polisi

Dk Msolla amewataka Wanayanga wasiyumbishwe na haya yanayoendelea, waweke mkazo katika malengo yao kuhakikisha wanakamilisha mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji pamoja na kutwaa ubingwa wa ligi kuu

"Sisi viongozi tunaamini Senzo hakufanya kosa lolote hivyo tutakuwa nae bega kwa bega na tutatoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha jambo hili linamalizika"

"Kwa mashabiki wetu ni muhimu kuwa wamoja, wasiyumbishwe na taarifa za mitaani. Tuna malengo mawili makubwa msimu huu kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu yetu pamoja na kutwaa ubingwa wa nchi," alisema Dk Msolla

Nae mshauri wa Yanga Senzo Mazingisa ameeleza kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Simba lakini ameahidi kuwa atashirikiana na Jeshi la Polisi katika uchunguzi wao ili kuhakikisha jambo hili linafika mwisho

Mapema leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Edward Bukombe alisema walimuhoji Senzo jana lakini aliachiwa huru bila ya masharti kwa kuwa hakuna kesi iliyofunguliwa dhidi yake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’