Baada ya mapumziko ya siku nne, kikosi cha Yanga kinarejea mazoezini leo kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Novemba 22 uwanja wa Benjamin Mkapa
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze aliwapa wachezaji mapumziko baada ya mchezo dhidi ya Simba ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Aidha mabingwa hao wa kihistoria, Jumapili Novemba 15 watakuwa na mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya African Lyon utakaopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Β
ADVERTISE HERE