Mshauri klabu ya Yanga Senzo Mazingisa leo amehojiwa na Jeshi la Polisi baada ya klabu ya Simba kumtuhumu kuihujumu
Inaelezwa Senzo anashikiliwa kutokana na Mawasiliano aliyofanya na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashabiki na Wanachama klabu ya Simba Hashim Mbaga ambaye alikamatwa hivi karibuni akituhumiwa na makosa hayo
Mbaga pamoja na wafanyakazi wengine waliokuwa na mawasiliano ya karibu na Senzo, walifutwa kazi hivi karibuni kwa tuhuma za kuihujumu Simba
Tangu alipojiunga na Yanga, ni kama ameacha sintofahamu upande wa pili, utulivu haupo
ADVERTISE HERE