Kiungo fundi wa Yanga Carlinhos amepona majeraha yaliyomuweka nje kwa zaidi ya wiki mbili na sasa anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha kocha Cedric Kaze kuelekea michezo ya ligi kuu baadae mwezi huu
Carinhos hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichoikabili Simba mwishoni mwa wiki iliyopita na kulazimishwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Kaze alimuondoa kikosini baada ya kuwa amefanya mazoezi kwa takribani siku mbili tu tangu apone majeraha
Yeye pamoja na Balama Mapinduzi ndio wachezaji pekee ambao hawajapata nafasi ya kukitumikia kikosi cha Kaze
Wakati alipotua nchini kuinoa Yanga, Kaze alimtaja Carlinhos kuwa mmoja wa wachezaji bora waliosajiliwa licha ya kuwa usajili wake hakuufahamu mapema
Kaze alisema Carlinhos ni mchezaji aliyekamilika kiufundi, kitu ambacho atataka kumuongezea ni kuimarisha 'Physique' yake ili awe na mchango mkubwa zaidi kwenye timu
Pengine mchezo wake wa kwanza unaweza kuwa dhidi ya Namungo Fc Novemba 22 uwanja wa Benjamin Mkapa pale ligi itakaporejea baada ya mapumziko ya kalenda ya CAF