Bao la Sarpong lasababisha kifo Mwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Nov 2020
Bao la Sarpong lasababisha kifo Mwanza

Bao la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga Jumamosi, limesababisha kifo cha shabiki kindakindaki wa Simba, Shaaban Jumanne β€˜Balwe’ wa jijini Mwanza, aliyefariki baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Taarifa za kifo cha Balwe, zimethibitishwa na Katibu wa Matawi ya Simba Mkoa wa Mwanza, Filbert Kabago ambaye alisema marehemu alifikwa na umauti akiwa katika kibandaumiza kwa Mwalimu Said, wakati akitazama mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu hizo za Kariakoo, Dar es Salaam, zilitoka sare ya kufungana bao 1-1

Kabago alisema kuwa mara baada ya Yanga kupata penalti baada ya winga wao, Tuisila Kisinda kufanyiwa madhambi eneo la hatari, marehemu alianza kujisikia vibaya kwa mwili kuishiwa nguvu na akajikongoja kutoka nje kupata hewa, lakini hali ikazidi kuwa mbaya na kufikwa na umauti.

Alisema marehemu alianza kutazama mchezo huo katika kibandaumiza kinachoitwa Vidumu kabla ya kuelekea kwa Mwalimu Said ambako ndiko umauti ulikomkuta.

Marehemu enzi zake alikuwa kipa makini, alizikwa Jumapili huko Mwanza na na mziko yake kuhudhuriwa na mashabiki na wanachama wa timu za Simba na Yanga jijini Mwanza

Bingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’