Mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari amesema kuzingatia mbinu walizopewa na kocha wao Cedric Kaze ni chanzo cha kuwanyima nafasi ya kung'ara nyota wa Simba Clatous Chama na Luis Miquissone kwenye mchezo wa watani ulioisha kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam juzi
Katika mchezo huo Yanga walicheza soka bora kipindi cha kwanza kwa kuwazuia nyota wa Simba waliozoeleka kuamua matokeo kwenye mechi nyingi zilizopita za ligi hiyo kushindwa kufurukuta.


Akizungumza baada ya kukamilika kwa mechi hiyo, Shomari alisema pamoja na kuzingatia mbinu hizo, lakini pia safu yao ya ulinzi ilikuwa makini kuziba nafasi ambazo wapinzani wao wangetumia kuwadhuru
"Mechi ilikuwa ngumu lakini upande wetu tumecheza kwa nidhamu kwa kuzingatia mbinu tulizopewa na kocha na tulifanikiwa kumzuia Chama na Luis kufungua ngome yetu"
Shomari hiyo ni mechi yake ya kwanza ya watani tangu amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Mtibwa Sugar lakini ameshukuru Mungu licha ya ugeni huo alionesha kiwango bora