Ukizungumzia mafundi wazawa eneo la kiungo sidhani kama yupo anayemfikia Feisal Salum 'Fei Toto'
Fei Toto amekuwa mchezaji tofauti sana msimu huu, kiwango chake kimeimarika sana lakini pia amekuwa kiakili
Katika kikosi cha Yanga kwa sasa Fei Toto ndio 'injini' ya timu, kocha Cedric Kaze amemuamini zaidi akimpa majukumu zaidi ya kucheza kiungo cha juu
Jana katika mchezo dhidi ya Simba yeye na Mukoko Tomombe ndio waliokuwa mabosi wa eneo la kiungo
Wamepeleka balaa Msimbazi kwani kuna wachezaji wanatuhumiwa na viongozi wao kuwa walicheza chini ya kiwango
Lakini ilikuwa kazi ya hawa mafundi wawili wakishirikiana na wenzao 'kupiga spana' eneo la kiungo
Huu utakuwa msimu mzuri sana kwa Fei Toto kama ataendeleza kasi hii aliyoanza nayo
Umri wake bado ni mdogo na pengine muda sio mrefu tutamshuhudia nchi za mbali akipeperusha bendera ya Tanzania