Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewataka viongozi wa Simba waache kutoa sababu zisizo na msingi pale timu yao inaposhindwa kupata matokeo
Baada ya mchezo wa jana ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1, klabu ya Simba kupitia kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Zacharia Hanspoppe, aliwatuhumu wachezaji Clatous Chama, Luis Miquissone na Larry Bwalya kuwa walicheza chini ya kiwango na kuwa watahitaji kuwachunguza
Mwakalebela amesema ni kawaida ya viongozi wa Simba kulalamika na kutoa shutuma pale wanaposhindwa
Amesema Yanga ilikuwa bora zaidi yao kimbinu na ndio maana wachezaji wao walishindwa kufurukuta
"Huyu Hanspoppe ni kawaida yake kulalamika na kuingilia mambo asiyoyajua. Sisi msimu huu tumejipanga, tuna kikosi imara kwa ajili ya kuchukua ubingwa"
"Timu yetu ilikuwa bora eneo la kiungo ndio maana wachezaji wao hawakufurukuta. Hivi kwa safu ile ya ulinzi wangepita wapi?," alihoji Mwakalebela
"Hata bao walilosawazisha ni makosa madogo tu ambayo tulifanya, sisi hatulaumu mtu kwa sababu tunafahamu ni sehemu ya mchezo"
Inaelezwa upo uwekezako mkubwa Chama akaachana na Simba mwishoni mwa msimu akiwa amegoma kuongeza mkataba
Amekuwa akihusishwa na kuungana na aliyekuwa CEO wa Simba Senzo Mazingisa aliyetimkia Yanga mapema msimu huu
Pengine hili ndilo linalowachanganya zaidi viongozi wa Simba na kufikia kumtuhumu kufanya hujuma katika mchezo huo
Hata hivyo uimara wa safu ya kiungo ya Yanga iliyokuwa chini ya Mukoko Tomombe na Feisal Salum pengine ndio sababu ya viungo wa Simba kupoteana
Mukoko ndiye aliyepewa tuzo ya nyota wa mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1