Tuisila Kisinda ni winga halisi na hakika hii mashine imefika wakati mwafaka ndani ya kikosi cha Yanga
Jana walinzi wa Simba walikuwa na wakati mgumu sana kumdhibiti hasa katika matukio ya mmoja kwa mmoja
Mkenya Joash Onyango ndiye aliyekuwa na wakati mgumu sana kukabiliana na Kisinda
Mkwaju wa penati waliopata Yanga ilikuwa zao la kasi ya TK Master ambaye alimzidi mbio Onyango na mkongwe huyo kumfanyia madhambi ndani ya eneo la hatari
Kuwekuwa na mjadala mkali kuhusu penati lakini ni wazi Onyango alianza kumfanyia madhambi Kisinda nje ya box lakini aliendelea kumshikilia hadi pale alipoingia ndani ya 18
Lakini vyovyote ilivyo, ipi ni tofauti na penati waliyopewa Simba kwenye mchezo dhidi ya Yanga uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 msimu uliopita?
Alichokifanya Meddie Kagere dhidi ya Kelvin Yondani katika mchezo ule sidhani kama kina tofauti na kilichofanyika kati ya Kisinda na Onyango
Yanga imeanza kurejea katika utamaduni wake wa kushambulia kupitia pembeni. Kocha Cedric Kaze anawatumia Kisinda na Farid Mussa kama mawinga halisi
Kaze anaendelea kukiimarisha kikosi chake, kwa hakika wakati utafika kuna watu maji wataita 'mma'