Msanii Juma Kassim Kirobota 'Nature' atakuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa kuwapa burudani mashabiki kabla ya mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa kuanzia saa 11 jioni
Mwananchi huyo atakuwa sambamba na wananchi wengine Kala Jeremiah, Bela Flava, Anita Mushi, Sholo Mwamba, Baby Madaha, Dullah Makabila na DJ Sweetlady
Aidha, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa wale walioshindwa kununua tiketi jana kutokana na changamoto ya mtandao, tatizo hilo limetatuliwa wawahi kununua tiketi zao asubuhi hii
"Tiketi zinaendelea kuuzwa. Wahi Tiketi yako mapemaa. Vibe kama lote. Juma Nature na TMK Wanaume atakuweoo leo kuinogesha Dar Derby," amesema Bumbuli
ADVERTISE HERE