Kiungo Haruna Niyonzima amerejea kikosini kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa keshokutwa Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Niyonzima alipata majeraha wakati Yanga ilipokuwa kanda ya ziwa akikosa mechi dhidi ya KMC, Biashara United na Gwambina Fc
Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda ameongeza nguvu katika kikosi cha kocha Cedric Kaze ambaye siku ya Jumamosi ataonja radha ya dabi ya Kariakoo
Yanga ilirejea jijini Dar es salaam juzi na moja kwa moja kuingia kambini kujiwinda na mchezo huo
Nyota mwingine Carlos Carlinhos ambaye alikuwa nje ya uwanja wa takribani wiki mbili, amejumuishwa katika kikosi kinachojiandaa kuikabili Simba
Hata hivyo Carlinhos huenda akakosa mchezo huo kwani hakufanya mazoezi na timu, alibaki jijini Dar es salaam wakati Yanga ilipokuwa kanda ya ziwa
Carlinhos alipata majeraha wakati Yanga ikijiandaa na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliopigwa Oktoba 22