Waamuzi sita kuchezesha Kariakoo Dabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2020
Waamuzi sita kuchezesha Kariakoo Dabi

Bodi ya ligi imebainisha kuwa waamuzi sita watatumika kwenye mchezo wa kwanza wa watani wa jadi msimu huu kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, Novemba 07 uwanja wa Taifa

Kuanzia msimu uliopita, TFF imeweka utaratibu wa kutumia waamuzi sita kwenye mchezo unaozikutanisha Yanga na Simba

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo amesema lengo la kutumia waamuzi sita ni kupunguza makosa na kuongeza umakini

Bado Bodi ya Ligi haijaweka hadharani majina ya waamuzi hao lakini zipo taarifa za kuwa wanaweza kuwa Martin Saanya, Ramadhan Kayoko, Abdallah Mwinyimkuu, Selemani Nonga na Abdulaziz Ally

Yanga inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mchezo huo wa kwanza msimu huu ambao awali ulipangwa kupigwa Oktoba 18 lakini ukasogezwa mbele

Mchezo umepangwa kupigwa kuanzia saa 11 jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’