Mlinda lango Metacha Mnata msimu huu amejihakikishia nafasi ya kuanza langoni mbele ya Farouk Shikhalo na Ramadhani Kabwili
Metacha amedhihirisha ni nguzo muhimu pale langoni, akiruhusu bao moja tu katika michezo nane aliyocheza
Kati ya hiyo, michezo saba amefanikiwa kutoruhusu bao lolote 'cleansheet'
Ni wazi kazi kubwa inafanywa na benchi la ufundi kuhakikisha Metacha pamoja na wenzake wanaendelea kuwa katika kiwango bora
Uimara wa Yanga umedhihiri mapema tu, Yanga ndio klabu yenye safu bora ya ulinzi msimu huu, wameruhusu mabao mawili tu katika michezo tisa
Bado Yanga haijapoteza mchezo wowote ndani ya ligi na hata mechi za kirafiki
ADVERTISE HERE