Alama saba kati ya tisa kanda ya ziwa sio haba - Senzo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2020
Alama saba kati ya tisa kanda ya ziwa sio haba - Senzo

Mshauri wa klabu ya Yanga Senzo Mazingisa amesema alama saba kati ya tisa walizopata kanda ya ziwa sio haba na sasa wamerejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba

Senzo ambaye anafanya kazi bega kwa bega na uongozi wa Yanga sambamba na GSM, amesema mechi walizocheza kanda ya ziwa hazikuwa nyepesi

"Tumekusanya alama saba kati ya tisa kanda ya ziwa sio haba. Haikuwa michezo rahisi. Tunarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo unaofuata. Yapo mengi tuliyojifunza, bado mapema, tutakabili kila mchezo kwa wakati," alisema

Ikiwa kanda ya ziwa, Yanga iliweza kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC kisha kuifunga Biashara United bao 1-0, timu hizo ziko katika nafasi tano za juu kwenye msimamo wa ligi

Jana mabingwa hao wa kihistoria wakalazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Gwambina Fc katika mchezo ambao kocha Cedric Kaze alifanya mabadiliko ya takribani wachezaji tisa kwenye kikosi chake kilichoanza

Kaze alichanga karata zake vyema kuhakikisha Jumamosi anakuwa na kikosi chake kamili na imara kuikabili Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’