Leo Wananchi wako Misungwi, jioni watashuka uwanja wa Gwambina kupepetana na wenyeji wao Gwambina Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Yanga inaendelea na kampeni yake ya kukusanya alama tatu tatu leo wakikumbana uso kwa uso na kocha wao wa zamani Mwinyi Zahera ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Gwambina Fc
Yanga ilitua Misungwi jana na wachezaji wakapata nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Gwambina
Ushindi au hata matokeo ya sare katika mchezo huo yataishuhudia Yanga ikipanda kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwaporomosha Azam Fc
Azam Fc na Yanga zote zina alama 22 lakini Azam Fc wamecheza mechi moja zaidi ya Yanga
Baada ya mchezo huo, Wananchi watarejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya watani zao Simba, siku ya Jumamosi, Novemba 07 2020