Utaratibu wa kutoa tuzo kwa wachezaji wanaofanya vizuri katika mechi, mwezi na kila msimu hutumiwa na vilabu vingi ikiwa njia moja ya kuwaongezea hamasa wachezaji
Msimu huu Yanga inatumia utaratibu huo kikamilifu ambapo tuzo ya mchezaji bora wa kila mechi hutolewa
Pia tuzo ya nyota wa mwezi inatolewa ambapo kiungo Mcongomani Mukoko Tomombe alikuwa mchezaji wa kwanza kupata tuzo hiyo kwa ajili ya mwezi wa tisa
Nyota walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora kwa ajili ya mwezi wa kumi ni Metacha Mnata, Bakari Nondo Mwamnyeto, Lamine Moro na Farid Mussa
Piga kura yako kupitia ukurasa rasmi wa klabu ya Yanga mtandao wa Twitter 'yangasc1935'
Β
ADVERTISE HERE