Mshambuliaji Yusufu Mhilu ameanza msimu kibabe akiwa miongoni mwa vinara wa mabao katika ligi kuu ya Vodacom
Akiwa amerejea hivi karibuni kutoka kwenye majeruhi, Mhilu ameweka kambani mabao manne ndani ya klabu yake ya Kagera Sugar
Hapa Yanga ilikosa uvumilivu kwa kumuachia aondoke kirahisi, huyu kijana ni mshambuliaji hasa. Msimu uliopita alimaliza ligi akiwa na mabao 14
Yanga ilijaribu kumrejesha usajili uliopita lakini yaonekana GSM hawakuweka mkazo mkubwa kuweza kumnasa na hivyo Kagera Sugar kufanikiwa kumuongezea mkataba
Mhilu amedhihirisha ni mshambuliaji mahiri, ameendelea kuimarika siku hadi siku
ADVERTISE HERE