Kwa misimu mitatu Yanga imelalamika juu ya hujuma nyingi walizokuwa wakifanyiwa kwenye ligi hasa kupitia waamuzi
Wengi wanakumbuka wakati wa Mwinyi Zahera, alizungumza waziwazi mbinu chafu zilizokuwa zikifanywa nje ya uwanja kuidhoofisha Yanga
Ni msimu huo ambao Simba walirundikiwa viporo 15, jambo hili historia imewekwa Tanzania kwani sidhani kama kuna ligi huko kwingineko timu moja imewahi kuwa na mechi za viporo 15
Hata msimu uliopita Simba ilinufaika zaidi na makosa ya waamuzi kulinganisha na timu nyingine
Walipolalamika Yanga walipuuzwa huku wengine wakitamba kuwa ni malalamiko hayo yalikuwa dalili ya kushindwa
Lakini inashangaza kuona msimu huu Simba nao wamekuwa vinara wa malalamiko
Jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji 'Mo' aliwatuhumu waamuzi kuwa wanaihujumu timu yake
Lakini pia baadhi ya waandishi wa habari wakaibua tuhuma kuwa Mshauri wa Yanga Senzo Mazingisa kuwa anashiriki kuwahujumu Simba
Mambo haya yote yameibuliwa kwa wakati mmoja ikionyesha dhahiri kuna ajenda imewekwa nyuma yake
Pamoja na uonevu mwingi ambao wamefanyiwa, Yanga wameamua kuacha kulalamika na badala yake wameunganisha nguvu kuhakikisha wanafanikiwa katika kila jambo lao
Ndio maana mpaka sasa timu pekee ambayo hajapoteza mchezo msimu huu ni Yanga
Sasa wameona kuna kila dalili msimu huu hawana chao, wanaanza kutengeneza propaganda kutafuta uhalali wa anguko linalowanyemelea