Msako wa alama tatu unaendelea Musoma leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Oct 2020
Msako wa alama tatu unaendelea Musoma leo

Kikosi cha Yanga leo kiko Mjini Musoma kuendelea na msako wa alama tatu saa kumi Alasiri wakitarajiwa kushuka uwanja wa Karume kuikabili Biashara United

Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kwani matokeo ya ushindi mnono yanaweza kuwashuhudia wakipanda kileleni mwa msimamo wa ligi

Azam Fc inayoongoza ligi ikiwa na alama 22, jana ilishikwa shati na JKT Tanzania kwa kulazimishwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Azam Fc imecheza mechi mbili zaidi ya Yanga

Kikosi cha Cedric Kaze kiliweka kambi mkoani Mwanza tangu walipopata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC wiki iliyopita

Yanga leo itashuka uwanjani bila ya nyota wake Carlinhos na Haruna Niyonzima ambao wote ni majeruhi

Mpaka sasa Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu, imeshinda mechi sita mfululizo na sare moja

Hii ni nafasi nyingine kwa mabingwa hao wa kihistoria kuendeleza umwamba wao msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’