Wakati wakiwa njiani kuelekea Musoma, msafara wa kikosi cha Yanga ulipata fursa ya kutembelea Makazi ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Muasisi wa Taifa la Tanzania
Msafara wa Yanga ukiongozwa na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla pia walipata nafasi ya kuonana na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyereere
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said akiwa sambamba na Dk Msolla, walimkabidhi Mama Maria jezi ya klabu ya Yanga


Inaelezwa hayati Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake alikuwa shabiki mkubwa wa klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE