Wanayanga wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwani klabu yao iko katika mikono salama ya watu ambao wana mapenzi makubwa nayo
Injinia Hersi Said na GSM kwa ujumla wanakeleza kwa vitendo kile walichowaahidi mashabiki wa Yanga msimu uliopita kuwa walaumiwe wao kama timu haitatwaa ubingwa msimu huu
Hersi yuko bega kwa bega na kikosi cha Yanga kila mahali wanapokwenda, kazi yake ni moja tu, kuhakikisha timu inapata kila wanachostahili ili kuhakikisha wanakamilisha wajibu wao ipasavyo
Kwa misimu ya karibuni Yanga ilikosa hamasa hii inayotolewa na GSM. Kwa hakika wachezaji wana deni kubwa kuhakikisha wanafanikisha malengo yaliyo mbele yao
ADVERTISE HERE