Sarpong aahidi kurejesha mabao Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Oct 2020
Sarpong aahidi kurejesha mabao Yanga

Mshambuliaji wa Yanga Michael Sarpong mpaka sasa amefunga mabao matatu katika mechi zote alizocheza pamoja na zile za kirafiki

Amefunga mabao mawili katika mechi za kirafiki na bao moja kwenye mchezo wa ligi kuu

Sio kasi ambayo Wanayanga walikuwa wakiisubiri kutoka kwake lakini mwenyewe amefunguka changamoto alizokutana nazo

"Najua kama mshambuliaji kazi yangu ni kufunga mabao, lakini muhimu zaidi ni kuisaidia timu kupata ushindi bila ya kujali nimefunga mimi au mwingine"

"Huu ndio msimu wangu wa kwanza kucheza ligi ya Tanzania, zipo changamoto nilizokutana nazo"

"Kikubwa nadhani kwa sasa niko tayari baada ya kuzoea mazingira, nitaipigania timu ili kuhakikisha tunakamilisha malengo yetu. Sina wasiwasi kwani najua nitafunga," alisema Sarpong

Sarpong alisababisha mkwaju wa penati kwenye mchezo dhidi ya KMC na Tuisila Kisinda kuirejesha timu mchezoni baada ya kuweka kambani tuta hilo

Aina ya uchezaji wake umewapa wakati mgumu walinzi wa timu pinzani kwani ni mshambuliaji mwenye 'physique' iliyoshiba kwelikweli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’