Kaze atafanya makubwa Yanga - Senzo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Oct 2020
Kaze atafanya makubwa Yanga - Senzo

Mshauri wa masuala ya uongozi na kiufundi ndani ya klabu ya Yanga, Senzo Mazingisa ameeleza furaha yake kufanya kazi ya kocha Cedric Kaze aliyetua hivi karibuni kuinoa Yanga

Mazingisa amefichua kuwa alitamani kufanya kazi na Kaze hata wakati alipokuwa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Kaze alikuwa chaguo lake la kwanza wakati wakitafuta mrithi wa Patrick Aussems

"Nimefurahishwa na utendaji wa Kaze kwa muda mfupi ambao tumekuwa nae ndani ya timu. Sasa tumeanza kuona ubora wa wachezaji tuliowasajili ambao hawakuwa wakionesha uwezo wakati wa kocha aliyepita," alisema Mazingisa

"Kaze ni kocha ambaye hata wakati nilipokuwa na klabu ya SImba tulimuhitaji lakini sikufanikiwa kumpata kwa sababu nilizidiwa na maamuzi ya wengi. Sio kazi rahisi kwa kocha wa kiafrika kuaminiwa na klabu kubwa kama Fc Barcelona lazima waliona kitu cha ziada kutoka kwake"

"Nafurahi niko nae hapa Yanga, matokeo aliyopata katika mechi mbili zilizopita ni ushahidi tosha kuwa ujio wake hapa ni uamuzi sahihi zaidi kufanywa na uongozi wa Yanga pamoja na wadhamini GSM"

"Nimehudhuria vipindi vya mazoezi, naona wachezaji viwango vyao vinaimarika tofauti na walivyokuwa chini ya kocha aliyepita. Yanga imesajili wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini viwango vyao viliporomoka kutokana na mbinu za kocha aliyepita, kila mchezaji alikuwa akicheza kivyake," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’