Kakolanya amvulia kofia Pondamali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2017
Kakolanya amvulia kofia Pondamali
Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya amesema, kwa kipindi kifupi alichokaa na kocha wake, Juma Pondamali, amejifunza mengi na hata ikitokea ameachana na klabu hiyo, ana vingi vya kujivunia.

Beno ambaye kwa sasa yupo kwenye hali ya sintofahamu kama anaweza kuendelea na Yanga au akaachana nao kutokana na kudai sehemu ya pesa zake ya usajili, mesema mafunzo anayoyapata kutoka kwa Pondamali ambaye ndiyo anawanoa makipa wote wa Yanga ni ngumu kwa timu pinzani kuwafunga, hata kama mechi hiyo ina presha kubwa.

"Aisee, Pondamali ni bonge la kocha na vitu viwili ambavyo najivunia kutoka kwake ni namna ya kupanga timu inaposhambuliwa na namna ya kuwasiliana na wenzangu hasa beki. Timu inaposhambuliwa kuna namna unatakiwa kuipanga na ikishinda pia kuna upangaji wake, hilo linasaidia Yanga kuwa imara zaidi na kutoyumbishwa na wapinzani,"alisema Kakolanya ambaye ameshindwa kutamba mbele ya Mcameroon Youth Rostand.

Ameongeza na kuzungumzia changamoto ya nafasi ya kucheza alisema: "Siku nikikaa golini tu, ushindani utaanza upya, itabaki kuwa kazi ya kocha kumuachia nani ampange kwenye mechi ili apate matokeo mazuri.Ò€

Kuhusu nafasi kwenye timu ya taifa alisema: "Majeruhi yaliyokuwa yananishumbua ndiyo tatizo, naamini wakiniona nacheza nitaitwa tu,ndio maana nimesema Yanga nikicheza ushindani utaanza upya,naendelea kujipanga na wala siwezi kukata tamaa."

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’