Baada ya kuifungia Yanga bao la ushindi dhidi ya KMC leo, Waziri Junior alionyesha maandishi ya fulana aliyovaa ndani akijitambulisha kama mfalme wa uwanja wa CCM Kirumba
Ndivyo ilivyo, huyu Junior ni mfalme wa dimba la CCM Kirumba na hakika benchi la ufundi la Yanga chini ya Cedric Kaze walifanya uamuzi sahihi wa kumpa nafasi leo
Takwimu zinaonyesha katika mechi 60 alizocheza kwenye ligi akiwana vilabu mbalimbali, Waziri amepachika mabao 34, ikiwa ni zaidi ya wastani wa kufunga bao moja kila baada ya mechi mbili
Bao alilofunga leo litamuongezea kujiamii na sasa ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwenye mechi zinazofuata
ADVERTISE HERE