Baada ya ushindi wa tano mfululizo ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Polisi Tanzania leo, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kupaa mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya KMC
Mchezo huo utapigwa uwanja wa CCM Kirumba, Jumapili October 25, 2020
Kampeni ya kuokota alama tatu kila mchezo inaendelea, uwanja wa CCM Kirumba ni uwanja mwingine wa nyumbani kwa Yanga
Hakuna shaka Wana Mwanza watajitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu
Yanga itakuwa na michezo mitatu kanda ya ziwa kabla ya kurejea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo dhidi ya Simba ambao unaweza kupigwa Novemba 07
Mechi nyingine mbili ambazo watacheza kanda ya ziwa ni dhidi ya Biashara United (October 30) na Gwambina Fc (Novemba 03)
ADVERTISE HERE