Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Uhuru
Mukoko Tomombe 'Teacher' ndiye aliyefunga bao la Yanga akimalizia pasi murua ya Farid Mussa akiwa ndani ya 18
Kwa nyakati tofauti wachezaji wa Yanga walionekana kuweka mpira chini, pasi nyingi za kuelekea mbele lakini walikabiliwa na upinzani kutoka kwa safu ya ulinzi ya Polisi Tanzania
Ugumu wa uwanja wa Uhuru inaweza kuwa changamoto nyingine ambayo kwa dhahiri ulionekana kuwatatiza wachezaji wa timu zote
Mpira ulikuwa haukai mguuni kwa urahisi

Upo mwanga wa aina ya timu ambayo Cedric Kaze anaitengeneza. Huu ni mchezo wake wa kwanza tangu aanze kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria siku nne zilizopita
Muhimu zaidi Yanga leo ilihitaji alama tatu. Ushindi umewapandisha juu kwenye nafasi ya pili wakiwashusha watani zao Simba ambao wamechezea kichapo mkoani Rukwa kwa kuchapwa bao 1-0 na Tanzania Prisons