Mapema leo kikosi cha Yanga kilipata nafasi ya kujifua kwenye uwanja wa Uhuru kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho Alhamisi
Mkufunzi wa mabingwa hao wa kihistoria Cedric Kaze kwa mara ya kwanza aliweza kutumia uwanja wa Uhuru ambao utatumika kesho kuiweka timu yake sawa kimbinu kuelekea mchezo huo
Kaze amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo, atawakosa wachezaji wanne ambao ni majeruhi
Wachezaji hao ni Abdulaziz Makame, Fahdi, Mapinduzi Balama na Carlinhos




ADVERTISE HERE