Sintofahamu imeendelea kutawala hatma ya mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba msimu huu ambao ulisogezwa mbele hadi Novemba 07 2020
Awali mchezo huo ulipangwa kupigwa Oktoba 18, lakini TFF wakausogeza mbele kwa kile walichoeleza wachezaji wa kigeni kuchelewa kurudi kutoka kwenye majukumu ya timu za Taifa
Taarifa za chinichini zimedai kuwa mchezo huo unaweza usipigwe Novemba 07 kutokana na timu za taifa kukabiliwa na mechi za kusaka tiketi ya michuano ya Afcon 2021 ambazo zitapigwa kati ya Novemba 09 na Novemba 18
Tanzania inapaswa kusafiri nchini Tunisia tayari kwa mchezo dhidi ya wenyeji wao hao ambao utapigwa Novemba 13
Ni wazi kabla ya safari hiyo Kocha Etienne Ndayoragije atahitaji angalau wiki moja kuiandaa timu yake
Lakini pia hata kwa wachezaji wa kigeni ambao wataitwa timu za Taifa wanaweza kuhitajika mapema kwa ajili ya maandalizi
Mechi hiyo inaweza kupigwa tena kalenda, taarifa zikibainisha kuwa unaweza kupigwa mwishoni mwa mwezi wa 12