Kaze aahidi kandanda safi la kushambulia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Oct 2020
Kaze aahidi kandanda safi la kushambulia

Kesho Alhamisi, Oktoba 22 kikosi cha mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga kitashuka dimba la Uhuru kumenyama na Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa kocha mkuu wa timu hiyo ya Wananchi, Cedric Kaze

Akiwa amewaandaa vijana wake kwa takribani siku tano, Kaze amebainisha nini Wanayanga watarajie kutoka kwa timu yao

Kaze amesema atapenda kuona timu yake ikicheza soka la kasi ambalo litasababisha wapinzani wao wafanye makosa mengi ambayo wao watayatumkia kuwaadhibu

"Tutacheza soka la kasi kwa sababu hii itawafanya wapinzani kufanya makosa mengi ambayo yatakuwa faida kwetu," alisema

Aidha Mrundi huyo ameongeza kuwa timu anayoiunda yeye haitakuwa tegemezi, wachezaji wote watakuwa na majukumu sawa uwanjani

Kaze amesisitiza kuwa atawapa nafasi wachezaji walionyesha nidhamu nzuri mazoezini, kuzingatia maelekezo na kujituma

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
27m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’