Afisa Msemaji na Mhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru kesho Alhamisi kuipa sapoti timu yao kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania
Mchezo huo umehamishwa kutoka uwanja wa Mkapa na utapigwa kuanzia saa kumi Alasiri
Nugaz amesema kwa muda ambao kocha Cedric Kaze ameinoa timu, mambo mazuri yameanza kuonekana
Amewaalika mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya aina yake kutoka kwa mabingwa wa kihistoria, Yanga

"Kwa namna ya siku mbili hizi mazoezi ya timu yetu yalivyokuwa, yananipa matumaini makubwa ya kukupa mualiko wa kuja Uwanja wa uhuru ili tuone kikosi chetu chini ya kocha wetu mpya Cedric Kaze"
"Ni Alhamis hii ya tarehe 22/10/2020 uwanja wa Uhuru dhidi ya Polisi Tanzania saa 10 kamili jioni kwa kiingilio cha Mzunguko 5,000 , B 10,000 na VIP A 15,000. Tukutane pale," ameandika Nugaz kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa kocha Kaze aliyeanza majukumu ya kuinoa Yanga Jumamosi iliyopita