Moja ya ahadi alizotoa kocha Cedric Kaze baada ya kutambulishwa kuwa kocha mkuu wa Yanga ni kutengeneza kikosi ambacho kitacheza kitimu zaidi
Kaze alisema hataangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, atahitaji kuunda timu ya wachezaji 11
Leo ikiwa siku ya nne tangu aanze kukinoa kikosi cha Yanga, Wanayanga watarajie mabadiliko makubwa ya uchezaji wa timu yao kadiri Mrundi huyo anavyendelea kuwapa 'madini' wachezaji wake

Katika mazoezi ya mabingwa hao wa kihistoria yanayofanyika uwanja vya Avic Town Kigamboni, Kaze hataki kuona mchezaji anakaa na mpira mguuni kwa muda mrefu
Ameanza kujenga utamaduni wa wachezaji kufanya maamuzi ya haraka wanapopata mpira na kuifanya timu isonge mbele kushambulia kwa haraka
Muda si mrefu Wanayanga wataanza kuishuhudia ile 'kampa-kampatena' iliyoasisiwa na Hans van Pluijm wakati akiinoa Yanga miaka mitano nyuma
Mabadiliko yanatarajiwa kuonekana keshokutwa pale uwanja wa Uhuru wakati Yanga itakapocheza na Polisi Tanzania..