Mechi za raundi ya sita ligi kuu ya Vodacom zinaendelea leo kwa mechi nne kupigwa katika viwanja mbalimbali
Maafande wa JKT Tanzania wao watakuwa nyumbani mkoani Dodoma kuikaribisha Tanzania Prisons katika mchezo ambao utapigwa saa nane mchana
Mechi nyingine ni kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Namungo Fc mkoani Morogoro, Coastal Union dhidi ya Biashara United mkoani Tanga na Polisi Tanzania dhidi ya Gwambina Fc mkoani Arusha

Mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga wao watasubiri mpaka Alhamisi, ndio watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kupepetana na Polisi Tanzania
Mchezo huo ambao utapigwa saa moja usiku, utakuwa mchezo wa kwanza kwa kocha Cedric Kaze aliyetua mwishoni mwa wiki iliyopita
ADVERTISE HERE