Yikpe 'katoboa' Arabuni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Oct 2020
Yikpe 'katoboa' Arabuni

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Yikpe Gnamien ameibukia huko Saudi Arabia baada ya kusajiliwa na Arar SC inayoshiriki ligi kuu nchini humo

Yikpe ni miongoni mwa wachezaji ambao walishindwa 'kutoboa' katika kikosi cha Yanga msimu huu baada ya kushindwa kuonyesha kiwango chenye ushawishi

Pamoja na kusaini mkataba wa miaka miwili mwezi Januari, mabosi wa Yanga walifikia makubaliano nae na hivyo kuvunja mkataba wake

Moja ya sifa kubwa aliyonayo Yikpe raia wa Ivory Coast, ni mpambanaji na haishangazi kuona ameweza kupata timu ndani ya muda mfupi licha ya kuwa alipokuwa hapa alionekana ni mchezaji ambaye hastahili kucheza hata timu ya daraja la kwanza

Jambo jingine ni kuwa watanzania tunaendelea kudhihirisha kuwa sisi tunafahamu sana soka kuliko wenzetu wengine huko duniani

Maana ni kawaida wachezaji wengi wanaoshindwa hapa, wanapoondoka hufanikiwa

Yikpe, David Molinga, Patrick Sibomana, Papy Tshishimbi ni miongoni mwa wachezaji walioachwa kwenye kikosi cha Yanga msimu huu

Molinga amesajiliwa na klabu ya Zesco United, Tshishimbi ametua AS Vita na Sibomana amerejea kwao Rwanda akisajiliwa na klabu ya Polisi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’