Burudani itaanza Alhamisi pale kwa Mkapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Oct 2020
Burudani itaanza Alhamisi pale kwa Mkapa

Alhamisi ijayo Oktoba 24 kikosi cha Yanga kitashuka dimba la Benjamin Mkapa kuikabili Polisi Tanzania ukiwa ni mchezo wa raundi ya saba ligi kuu ya Vodacom

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze aliyetua juzi usiku na jana akasaini mkataba wa miaka miwili

Raia huyo wa Burundi leo anatarajiwa kuanza kuwanoa vijana wake, akiahidi mabadiliko ya uchezaji wa timu yake mapema tu kwenye mchezo wake huo wa kwanza

"Tutakuwa na siku nne za maandalizi kabla ya mchezo wetu unaofuata. Natarajia kuwa na vipindi saba vya mazoezi. Ni muda mchache lakini mashabiki watarajie kuanza kushuhudia mabadiliko namna vile tutakavyokuwa tukicheza," alisema Kaze ambaye tayari ametua Kigamboni kuanza majukumu yake

Kaze aka 'Guardiola wa Kirundi' ameweka bayana kuwa anataka kuiona timu yake ikicheza mbali zaidi ya lango lake na kuwa vijana wake wanapaswa kumiliki mchezo kwa muda wote

Ni mfumo ambao utahitaji wachezaji kuwa timamu kwelikweli kwani mbinu hii inawafanya wacheze pamoja wanaposhambulia na hata wakati wa kuzuia

Mpango wa mfumo huu ulianza kutekelezwa mapema na kocha msaidizi Juma Mwambusi ambaye baada ya Zlatko Krmpotic kutimuliwa, aliwaongezea wachezaji muda wa kufanya mazoezi, wakijifua mara mbili kwa siku lengo likiwa kuwafanya wawe na uwezo wa kucheza dakika 120 bila ya kuchoka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’