Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze ameeleza furaha yake baada ya kuwasili nchini kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Kaze alitua majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo na kupokewa na Mhandisi Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, viongozi wa Yanga na mashabiki waliojitokeza kwa wingi JNIA


"Ni heshima kubwa kwangu kujiunga na Yanga, timu yenye historia kubwa hapa Tanzania na Barani Afrika. Baada ya kutangazwa kuwa kocha wa Yanga nilipata pongezi nyingi kutoka kila pembe ya dunia. Nilishangaa kuona Yanga ni brand kubwa sana"
"Nawashukuru Wanayanga kwa mapokezi yenu, nimekuja hapa kushirikiana nanyi kuhakikisha tunakamilisha malengo tuliyojiwekea," alisema Kaze
Kocha huyo anayezungumza kwa ufasaha lugha za Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani na Kireno, amesema kusudio lililomleta hapa nchini ni kuhakikisha anashinda mataji
"Kwa ukubwa wa Yanga hakuna tageti zaidi ya kushinda ubingwa. Kama kunakuwa na tageti tofauti basi hiyo sio Yanga..."

Kaze amesema ataanza rasmi program za mazoezi kesho Jumamosi na anatarajia kuwa na vipindi saba vya mazoezi kabla ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Jumatano ijayo