Nimekuja Yanga kufanya kazi - Ntibazonkiza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2020
Nimekuja Yanga kufanya kazi - Ntibazonkiza

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Said Ntibazonkiza amesema ujio wake Yanga ni kwa ajili ya kazi moja tu, kuhakikisha anawasaidia mabingwa hao wa kihistoria kushinda mataji

Ntibazonkiza alisajiliwa na Yanga mapema wiki hii kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akiw amchezjai huru Yanga ikimnasa baada ya kumalizika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya Burundi uliomalizika kwa Burundi kupata ushindi wa bao 1-0 ambalo aliliweka kambani yeye

Ntibazonkiza amekiri ujio wake Yanga una mkono wa kocha mpya wa timu hiyo Cedric Kaze ambaye aliwahi kumfundisha kwenye timu ya Taifa mwaka 2011

"Mimi nimekuja Yanga sio kwa bahati mbaya, wapo wanaofikiria nimesajiliwa baada ya mchezo dhidi ya Tanzania. Tulikuwa na mazungumzo na Yanga miezi miwili au mitatu nyuma lakini nilishindwa kujiunga nao kutokana na changamoto kadhaa zilizokuwepo wakati huo. Sasa nilipokuja tena hapa ikawa rahisi kumalizana nao kwani hata yale yaliyotukwamisha mwanzo hayapo," amesema

"Nimekuwa nikiwasiliana na kocha Kaze mara kwa mara hata kabla mpango wa kujiunga na Yanga haujaibuka. Kabla sijasaini mkataba, alinipigia simu na kunielekeza ananihitaji hivyo niwasikilize viongozi wa Yanga. Nimezungumza nae pia baada ya kusaini amenieleza mipango yake hapa"

Ntibazonkiza ataanza kuitumikia Yanga mwezi Disemba pale dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa lakini atakuwa na muda wa kuzoeana na wenzake kwani ataanza kujifua na mabingwa hao wa kihistoria Novemba 15 siku ambayo mkataba wake utaanza rasmi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’